11.08.07 Interview met Mai Mai Bevelhebber Paluku Jackson (BLO)

{
window.open('http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&do_pdf=1&id=703','win2','status=no,toolbar=no,scrollbars=yes,titlebar=no,menubar=no,resizable=yes,width=640,height=480,directories=no,location=no'); return false;
}" href="http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&do_pdf=1&id=703" target="_blank">
 
{
window.open('http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&task=view&id=703&pop=1&page=0&Itemid=2','win2','status=no,toolbar=no,scrollbars=yes,titlebar=no,menubar=no,resizable=yes,width=640,height=480,directories=no,location=no'); return false;
}" href="http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&task=view&id=703&pop=1&page=0&Itemid=2" target="_blank">
 
{
window.open('http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&task=emailform&id=703&itemid=2','win2','status=no,toolbar=no,scrollbars=yes,titlebar=no,menubar=no,resizable=yes,width=400,height=250,directories=no,location=no'); return false;
}" href="http://www.benilubero.com/index2.php?option=com_content&task=emailform&id=703&itemid=2" target="_blank">
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Beni-Lubero Online (BLO) : Amjambo Afande Jackson !

 
Commandant ( Cmdt)  Jackson : Muzuri sana!
 
BLO : Habari toka Mbingi zasema kwamba Afande Mai-Mai Jackson na Lafontaine wanapambana katika mapigano makali. Kwa nini mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe ?
 
Cmdt Jackson : Hata mimi sijui kwa nini Lafontaine anaganisha Brigade Baleine ambayo inajitayarisha kwa brassage. Sijui sababu gani Lafontaine anaharibu mahali alipozaliwa.
 
BLO : Ni kweli kwamba umekataa kuwasiliana naye katika uongozi wa Brigade Baleine ?
 
Cmdt Jackson : Huo ni uongo mtupu ! Wakati tulianzisha Brigade Baleine, Lafontaine hakukuwepo. Na kama anatufuta kutumika nasi, tutamukaribisha mikono miwili. Alakini mpaka leo mimi sijapata ujumbe hata moja kutoka kwa Lafontaine kutuomba chochote.  Habari toka kwake ni vita, uporaji wa mali ya raia kama alivyo fanya Mbingi samedi iliyopita. Namna gani utawasiliana na mtu kama huyo?
 
BLO : Kuwazo yako, Lafontaine anatafuta nini ? Kwa nini anapiganisha Brigade Baleine kuliko Brigade za Nkunda?
 
Cmdt Jackson : Sijui ! Inaonekana Lafontaine anachuki kwani wa Mai-Mai wa Mbingi walimukataa baada ya kuua Commandant wao Delemba. Inawezakana Lafontaine aliyekuwa anajidai kuwa leader wa Mai-Mai wa Nord-Kivu, amesikia haya kwani hakuna Mai-Mai ambaye amemusamehe kwa mauaji kinyama ya Commandant Delemba. Lafontaine  kujiunga na FDLR, na NKunda, na vikosi ambavyo vinaharibu usalama wa Nord-Kivu ni jambo ambalo limetuacha hoi sisi wote.
 
BLO : Afande Jackson, Ujumbe wako kwa Lafontaine ni upi ?
 
Cmdt Jackson : Lafontaine ni rafiki toka zamani. Tulitumika pamoja naye. Lafontaine akaamua kuenda Kinshasa kutafuta pete za ujemadari  katika jeshi la Congo. Sasa yeye ni Colonel. Sisi tukabaki mjini tukipambana na adui. Ujumbe wangu kwa Lafontaine, ni kwamba aweke silaha chini ili sisi watoto wa Nord-Kivu tujiunge mkono kusudi raia apate tena usalama.
 
BLO : Unawaza ni nani anaweza kurudisha amani kati yako na Lafontaine ?
 
Cmdt Jackson: Nafikiri kuna watu wengi ambao wanaweza kazi hiyo. Kitu ya kwanza ni kuweka kwanza silaha chini na kuenda mahali pa neutre kama Butembo, Musienene, Kyondo, ao eneo lingine la Beni-Lubero, etc.
 
BLO: Kwa nini hautaje Goma mahali kuna wakuu wa Jeshi la Nord-Kivu? 
.
Cmdt Jackson : Sitaje Goma kwani ni mbali na mahali Brigade Baleine iko.Na vile uwasiliano wango wa na Lafontaine ni uwasiliano wa kindugu siyo wa kijeshi. Nafikiri kwamba ni wazazi ao wazee wa Beni-Lubero wanaweza kutupatanisha kama ndugu kabla ya kuongea kijeshi.
 
BLO: Ni mtu gani anaweza kurudisha  umoja kati yako na Lafontaine?
 
Cmdt Jackson: Hii ni swali ngumu kwani siwezi kuamua peke yangu. Mimi naweza kutoa majina ya watu Fulani Fulani… Inafaa vile vile Lafontaine atoe maoni na pendekezo zake. Alakini sijui kama Lafontaine anatafuta uwasiliano huo kwani tayari yeye amejiunga na watu ambao hawapendi usalama wa Nord-Kivu.
 
BLO: Kati ya Gouverneur wa Nord-Kivu, Commandant mkuu  wa Jeshi la jimbo la Nord-Kivu, Monuc, wazee wa makanisa mbalimbali, Société civile, chefs coutumiers, … unaweza kuchagua nani kama mpatanishi ?
 
Cmdt Jackson: Mimi sina shida ya mpatanishi. Yeyote anayeweza kusaidia ili amani irudi Nord-Kivu, nitamuunga mkono.
 
BLO :  Habari toka Rutshuru zasema kwamba  vikosi vya Nkunda vinatarajia kuvamia territoire za Lubero na Beni. Brigade Baleine inajiandaa namna gani kwa vita hivi?
 
Cmdt Jackson: Brigade Baleine haina mpango wa kufanya vita. Ukomo wa Brigade Baleine ni kuwakusanya wa Mai-Mai wote wa Lubero ili waende Brassage, wafanye jeshi moja la Congo. Hii ndio kazi nimepewa na Jemadari mkuu wa Huitième Région Militaire. Kama kuna vita fulani, ni kwa wakuu wa jeshi kuamua..
 
BLO : Msaada gani unapata toka kwa wakuu wa Jeshi wa Jimbo la Nord-Kivu ?
 
Cmdt Jackson: Tunapewa chakula, alakini haikitoshe.. Wa Mai-Mai wamekuwa wengi. Sasa tuna zaidi ya vijana elfu moja ambao bado wanakomaa nawanao hitaji chakula. Tumeomba vile matibabu, alakini hatuja pata jibu. Mpaka sasa vijana wanahitaji tu chakula na matibabu ili wapiganie usalama wa inchi yao. Hatutafute kujifanya matajiri ao cheo fulani katika serikali. Nia yetu sasa ni kutumikia inchi yetu. Tumaini letu ni kwamba raia wa Nord-Kivu vile watatusaidia ili tuwatetee vizuri
 
BLO : Unaomba nini kwa wakaaji wa Beni-Lubero ?
 
Cmdt Jackson : Tunawaomba waelewe vizuri nia yetu, wajue kwamba Mai-Mai si adui yao ila wakombozi wao. Aliye na chakula, dawa, nguo, kiatu, hema, atuletee hapa Mbingi ao mahali pengine tulipo ili tutimize kazi yetu vizuri. Wakijua mahaliwa Mai-Mai ambao hawapendi brassage wanafichama, watujulishe ili tuwaunganishe nasi. Tukijiunga pamoja tutafanya kazi vizuri.
 
BLO : Siku gani Brigade Baleine itaenda Brassage ?
 
Cmdt Jackson : Ilo ni swala la kuuliza Jemadari wa Jeshi la Nord-Kivu na wakubwa wa Monuc. Sisi tuko tayari kuenda Brassage. Tatizo letu sasa ni chakula na matibabu ! Watoto wana njaa! Waliosoma wanasema kama : " Ventre affamé n'a point d'oreilles". Kuwapa moyo wa kuenda Rumangabo ao mahali pengine kwa brassage, inatuomba tuwapatie chakula sasa.
 
BLO : Asante sana Afande Jackson kwa kujibu maswali yetu.
 
Cmdt Jackson : Aksanti sana !
 . 
Interview réalisée au téléphone le 8 Août 2007 par Kakule Mathe  pour le compte de Beni-Lubero Online.

Leave a Comment

You must be logged in to post a comment.